Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga kwa niaba ya Mhe.Waziri Mkuu dkt.Mwigulu Nchemba amekabidhi kiti mwendo kwa kijana mwenye ulemavu Martin Joseph mkazi wa Babati,baada ya familia ya kijana huyo kuomba msaada kwa waziri mkuu alipokuwa kwenye ziara yake mwezi machi /2026 mkoani humo.

Akizungumza baada ya kukabidhi kiti mwendo hicho Sendiga amewataka wazazi wa kijana huyo kukitunza na kuhakikisha wanampeleka kwenye matibabu kwa kuwa Serikali imetoa barua maalum ya msamaha wa matibabu kwa kijana huyo.
kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara dkt.Andrew Method amesema kupitia mpango wa bima ya afya kwa wote kijana huyo atapatiwa kadi ya matibabu katika utaratibu wa watu wenye ulemavu.
Aidha mama mzazi wa kijana huyo Anastazia Sulle ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kupatiwa msaada huo.
