MRADI WA KUSAFIRISHA UMEME KUTOKA IRINGA-SUMBAWANGA KUINUA UCHUMI WA WANANCHI

NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI

Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Mashaka Biteko ameweka jiwe la msingi katika Mradi wa kusafirisha Umeme Kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzaniaa na Zambia(TAZA) hatua itakayosaidia kuinua Uchumi kupitia Nishati.

Tangu Mkoa wa Rukwa kuanza ulikuwa ukitumia Umeme kutoka Nchi Jirani ya Zambia ambao Serikali ilikuwa ikitumia zaidi ya Bilioni 15  kwa Mwaka kama Gharama ya malipo ya Umeme kuuhudumia Mkoa huo ,ujio wa Naibu Waziri mkuu mkoani rukwa umelenga kuja kuweka jiwe la msingi katika mradi Mkubwa wa kuunganisha Umeme wa Gridi ya Taifa  hatua inayolenga kuwezesha upatikanaji wa Nishati ya uhakika ili kukuza Sekta ya Viwanda na Biashara.

Mkurugenzi Mtendaji Tanesco   ameeleza kuwa Mradi huo unaenda kuunganisha Nchi za Afrika katika upatikanaji wa Nishati ya Umeme ambapo pia Tanzania itaweza kuwa na uwezo wa kusambaza umeme Nchini nyingine za Afrika zinazounganishwa na jumuiya ya afrika kusini na afrika mashariki.

Kwa upane wake Viongozi wawakilishi wa Wananchi wametoa pongezi kwa hatua inayofanyika na Serikali

Ujenzi wa njia ya kusafirisa umeme yenye urefu wa Kilomita  616 kutoka Mkoa wa Iringa kuifikia Mkoa wa Rukwa unaghalimu kiasi cha fedha za Kitanzania Bilioni 517 umeanza ambapo tayari  hatua za awali za kuanza ujenzi Vituo vya kupozea Umeme katika maeneo ya Tagamenda,Kisanda,Iganjo,Nkangamo na Malangali umeanza.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.