SOKO KUU WILAYA YA MASASI LATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO

Soko la Mji wa Masasi

     Soko Kuu la Mji Masasi (Mkuti) limeteketea kwa Moto usiku wa kuamkia leo Julai 17,2024 kuanzia majira ya saa 4 usiku na kuathiri upande wa eneo la Mauzo ya Samaki pamoja na kusababisha hasara kubwa kwa Wafanyabiashara wa Soko hilo.

      Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Maafisa Uchunguzi wa Maafa bado hawajatoa taarifa kamili kuhusu chanzo cha Moto huo japo mashuhuda wameeleza kuwa ni Shoti ya Umeme ambapo ni baada ya umeme kukatika na kurudi kwa nguvu kubwa na kushindwa kuuhimili

      Moto huo umewaka kwa takribani masaa matatu mpaka kufikia majira ya Saa 7 Usiku na baadhi ya mashuhuda wameeleza hali iliyopo katika Soko hilo kwa sasa hairidhishi na wameiomba Serikali iwafikirie katika hilo.

 

hot
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.