ZANZIBAR INAENDELEA KUPIGA HATUA KWENYE SEKTA YA UTALII KIMATAIFA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Dkt. Aboud Suleiman Jumbe
English

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Dkt. Aboud Suleiman Jumbe Akizungumza katika tathmini ya utekelezaji wa siku 100, amesema Zanzibar imeendelea kufanya vizuri na kujipatia nafasi kwenye orodha mbalimbali za kimataifa za utalii.

Ameeleza kuwa Zanzibar sasa ipo katika kumi bora barani Afrika kwenye vivutio vya utalii, miradi bora ya kitalii, maeneo bora ya honeymoon pamoja na michezo ya baharini, hali inayoongeza ushindani na kuimarisha nafasi ya Zanzibar katika soko la kimataifa la utalii.

Aidha, amesema Tanzania ina kifurushi kamili cha utalii, ambapo wageni hutembelea hifadhi za taifa na kukamilisha safari zao Zanzibar. Kuhusu uwekezaji, amesema gharama za kuwekeza Zanzibar bado ni nafuu ikilinganishwa na baadhi ya nchi washindani, hali inayozidi kuvutia wawekezaji wa kimataifa.

Mafanikio haya ni sehemu ya matokeo ya uongozi thabiti wa Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndani ya siku 100 za utekelezaji wa vipaumbele vya maendeleo. 

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.