Vijana waliomaliza Mafunzo ya U/Riport wametakiwa kuwa Mabalozi kwa Vijana Wenzao katika kuwajengea uwezo kupitia fursa wanazozipata kutoka Taasisi mbalimbali.
Akizungumza katika Mkutano wa Kuwaaga Vijana Mabalozi wa Program hiyo katika Ukumbi wa Takwimu Mazizini Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana Shaib Ibrahim Wizara ya Habari imeamuwa kujenga Vituo Vinne vitakavyotowa Taaluma kupitia Vijana hao kwa lengo la kuwajenga Kitaaluma
Akisoma Risala Balozi wa Mradi wa U/Report Sara Abdalla Moh'd amesema wamekuwa wakitowa nafasi mbalimbali za ushiriki wa maendeleo ya Vijana pamoja na Mabalozi katika kuwapa ujuzi wa Elimu ya Afya na Ajira
Mratibu wa Mradi huo hapa Zanzibar Sheila Makungu Mwinyi amefahamisha kuwa kuanzishwa kwa Program ya Mabalozi hao kuna lengo la kuwashirikisha Vijana na kuwawezesha kupata Miradi ya Mikopo pamoja na kuazisha Vikundi vya Maendeleo
Jumla ya Mabalozi 20 kutoka Unguja na Pemba wamemaliza Mafunzo ya Program ya U/Report kwa Muda wa Miaka Sita kuanzia 2018 Hadi 2024 ambapo wamepatiwa Vyeti vya kuhitimu Mafunzo hayo.