TAWIA YATOA MSAADA KWA WATOTO 40 WANAOSUMBULIWA NA TATIZO LA SARATANI

MSAADA KCMC

   Shirika lisilo la Kiserikali  Tanzania Windon Association (Tawia) linalojihusisha na kutetea haki za Wajane limetoa Msaada wa vitu mbali mbali kwa Watoto 40 wenye Maradhi ya Saratani ya Macho , Damu, Figo, Mifupa  katika Hospitali ya  Rufaa ya KCMC Moshi.

   Mratibu wa Shirika hilo Kanda ya Kaskazini Messe Ndosi amesema Msaada huo utawasaidia Wazazi wenye Watoto hao ili na wao wajione kama Watoto wengine wasiokuwa na matatizo hayo.

   Muuguzi katika Kitengo cha Saratani kwa Watoto pamoja na Watu Wazima katika Hospitali hiyo Dkt.Lucas  amesema kuna matatizo mbali mbali kwa Wazazi kwa kushindwa kuwapatia baadhi ya huduma hivyo Wadau hao wanapopatikana ni vyema kusaidia Wagonjwa ili kupata Faraja kwa Wagonjwa hao..

   Baadhi ya Wazazi ambao wana Watoto Wagonjwa katika Hospitali hiyo wamelishukuru Shirika hilo kwa msaada waliowapatia pamoja na Hospitali hiyo kuwapa huduma.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.