WANANCHI WA VIJIJI VYA MTAKUJA KIJINI NA DODOMA WALILIA UKOSEFU WA HUDUMA UMEME

UMEME

   Wananchi wa Vijiji vya Dodoma na mtakuja Jimbo la Kijini Mkoa wa Kaskazini Unguja wamelalamikia ukosefu wa huduma ya Nishati ya Umeme inayokwamisha shughuli za Maendeleo ya Kijiji hicho.

    Katika Vijiji vya Mtakuja na dodoma vyenye Wakaazi zaidi ya 200 Wananchi wa Maeneo haya wameiomba Serekali kuwaharakishia huduma ya Umeme ambayo itapeleka mbele Maendeleo ya Vijiji hivi katika harakati zao.

    Wamesema licha ya Mamlaka husika kuanza kupeleka huduma za Awali za kuunganisha Umeme  Wananchi hao wameeleza Wasiwasi  wao wa kutokamilika kwa huduma hiyo kwa wakati uliopangwa

   Mbunge wa Jimbo la Kijini Matemwe Mhe.Yahya Ali Khamis amekiri kuwepo kwa matatizo hayo katika Vijiji hivyo na ameiomba Serekali kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo

   Akitoa ufafanuzi wa Tatizo hilo Mkuu wa Divishen ya Ugavi ZECO Mhandisi Yussuf Hamadi Omar amesema Serikali imekusudia  kuimarisha huduma ya Nishati  kila Kijiji hivyo amewahimiza Wananchi wa Vijiji hivyo kuwa wastahamilizu huku Serikali inalitafutia ufumbuzi tatizo hilo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.