Wananchi wa Vijiji vya Dodoma na mtakuja Jimbo la Kijini Mkoa wa Kaskazini Unguja wamelalamikia ukosefu wa huduma ya Nishati ya Umeme inayokwamisha shughuli za Maendeleo ya Kijiji hicho.
Katika Vijiji vya Mtakuja na dodoma vyenye Wakaazi zaidi ya 200 Wananchi wa Maeneo haya wameiomba Serekali kuwaharakishia huduma ya Umeme ambayo itapeleka mbele Maendeleo ya Vijiji hivi katika harakati zao.
Wamesema licha ya Mamlaka husika kuanza kupeleka huduma za Awali za kuunganisha Umeme Wananchi hao wameeleza Wasiwasi wao wa kutokamilika kwa huduma hiyo kwa wakati uliopangwa
Mbunge wa Jimbo la Kijini Matemwe Mhe.Yahya Ali Khamis amekiri kuwepo kwa matatizo hayo katika Vijiji hivyo na ameiomba Serekali kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo
Akitoa ufafanuzi wa Tatizo hilo Mkuu wa Divishen ya Ugavi ZECO Mhandisi Yussuf Hamadi Omar amesema Serikali imekusudia kuimarisha huduma ya Nishati kila Kijiji hivyo amewahimiza Wananchi wa Vijiji hivyo kuwa wastahamilizu huku Serikali inalitafutia ufumbuzi tatizo hilo.