SHETTA AIWAKILISHA DAR ES SALAAM KATIKA JUKWAA LA UONGOZI WA MAMEYA AFRIKA

Meya wa Jiji la Dar es Salaam Nurdin Bilal Maarufu kama 'Shetta'
English

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Nurdin Bilal Juma (Shetta), kwa sasa yupo Cape Town, Afrika Kusini, akishiriki katika mkutano wa African Mayoral Leadership Initiative (AMALI) unaowakutanisha mameya na viongozi wa miji kutoka barani Afrika.

Katika mkutano huo, Mstahiki Meya alipata fursa ya kuwasilisha maono ya urithi wa uongozi (legacy pitch) kwa niaba ya Jiji la Dar es Salaam akiweka mbele ajenda ya maendeleo jumuishi, ajira kwa vijana, na uongozi wa miji unaozingatia watu.

Katika uwasilishaji wake, Meya Shetta alisisitiza dhamira ya Jiji la Dar es Salaam kuunda ajira 300,000 ifikapo mwaka 2030, kupitia uwekezaji kwenye mafunzo ya ujuzi kwa vijana, mikopo ya jiji inayosimamiwa kwa uwazi na ufanisi, pamoja na ushirikiano thabiti na Serikali Kuu.

 

Ameeleza kuwa maendeleo ya miji hayapaswi kupimwa kwa miundombinu pekee, bali kwa athari chanya kwa maisha ya wananchi, hususan vijana na makundi yaliyo katika mazingira magumu. Ushiriki wa Dar es Salaam katika mkutano wa AMALI unaonesha dhamira ya jiji kujifunza, kushirikiana, na kuchangia uzoefu wake katika kujenga miji yenye fursa, usawa, na ustawi kwa wote barani Afrika

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.