SHETTA AIWAKILISHA DAR ES SALAAM KATIKA JUKWAA LA UONGOZI WA MAMEYA AFRIKA
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Nurdin Bilal Juma (Shetta), kwa sasa yupo Cape Town, Afrika Kusini, akishiriki katika mkutano wa African Mayoral Leadership Initiative (AMALI) unaowakutanisha mameya na viongozi wa miji kutoka barani Afrika.
Katika mkutano huo, Mstahiki Meya alipata fursa ya kuwasilisha maono ya urithi wa uongozi (legacy pitch) kwa niaba ya Jiji la Dar es Salaam akiweka mbele ajenda ya maendeleo jumuishi, ajira kwa vijana, na uongozi wa miji unaozingatia watu.
