MAMA SAMIA NI KIONGOZI WA MFANO WA MAENDEELEO

WAMAMA WALIOJIFUNGUA
English

Akinamama waliojifungua katika Hospital ya Wilaya Vitongoji Chake Chake Kituo cha Afya Kendwa na Tundauwa, wamesema Dkt. Samia ni Kiongozi imara na mwenye maono makubwa katika kuileta Nchi maendeleo.

Akinamama hao wameyasema hayo kwa nyakati tofauti mara baada ya kupokea zawadi kutoka  Ofisi ya CCM uratibu Pemba kwa akina mama hao

Waliyojifungua ikiwa ni kusherekea Siku ya Kuzaliwa ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano  wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan .

Wamesema wamefarajika kwa kiasi kikubwa kupatia msaada huo ,huku wakiitaka Jamii kuendelea kutunza amani na utulivu  na kuweza kuwaunga mkono  Viongozi walioko Madarakani ili kupata maendeleo zaidi.

Wakizungumza na akina Mama hao  Maafisa Ofisi ya Uratibu CCM  Pemba Ndg. Rahima Khamis Haji na Tatu Kassim Ali  wamesema lengo la  Ziara hiyo ni kuweza kuwafaraji akinamama waliojifungua ili kiweza kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusherekea Siku yake ya Kuzaliwa huku wakiwataka akinamama hao kujitahidi kusimamia malezi ya Watoto wao ili kupata  Viongozi wazuri wa baadae.

Nao Wauguzi wamekipongeza Chama cha Mapindunzi kwa kuwaunga mkono akinamama mara tuu baada ya kujifunguwa.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.