Akinamama waliojifungua katika Hospital ya Wilaya Vitongoji Chake Chake Kituo cha Afya Kendwa na Tundauwa, wamesema Dkt. Samia ni Kiongozi imara na mwenye maono makubwa katika kuileta Nchi maendeleo.
Akinamama hao wameyasema hayo kwa nyakati tofauti mara baada ya kupokea zawadi kutoka Ofisi ya CCM uratibu Pemba kwa akina mama hao
Waliyojifungua ikiwa ni kusherekea Siku ya Kuzaliwa ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan .
Wamesema wamefarajika kwa kiasi kikubwa kupatia msaada huo ,huku wakiitaka Jamii kuendelea kutunza amani na utulivu na kuweza kuwaunga mkono Viongozi walioko Madarakani ili kupata maendeleo zaidi.
Wakizungumza na akina Mama hao Maafisa Ofisi ya Uratibu CCM Pemba Ndg. Rahima Khamis Haji na Tatu Kassim Ali wamesema lengo la Ziara hiyo ni kuweza kuwafaraji akinamama waliojifungua ili kiweza kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusherekea Siku yake ya Kuzaliwa huku wakiwataka akinamama hao kujitahidi kusimamia malezi ya Watoto wao ili kupata Viongozi wazuri wa baadae.
Nao Wauguzi wamekipongeza Chama cha Mapindunzi kwa kuwaunga mkono akinamama mara tuu baada ya kujifunguwa.



