Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale inatarajia kufanya maonyesho ya Utalii na Uwekezaji katika Viwanja Dimani ili kuiinua Zanzibar Kiuchumi kupitia sekta ya Utalii.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mh Mudrik Ramadhan Soraga amesema kukuza uwekezaji katika Visiwa vya Unguja na Pemba ni kutoa fursa kwa wadau wa utalii na kujiongezea kipato.
Aidha Waziri Soraga amesema maonesho hayo ni hatua muhimu katika kuiweka Zanzibar kwenye Ramani ya Dunia kama eneo lenye fursa za kipekee za kuwekeza ili kuweka kumbukumbu za kudumu na kuchangia kutunza, kuhifadhi na kuimarisha Utamaduni .
Maonesho hayo yatakayohudhuriwa na zaidi Wadau wa Utalii Mia Mbili 50 yanatarajiwa kufanyika tarehe 25 na 26 Oktoba ambapo Kauli Mbiu ni “Kukuza Utalii Endelevu, Uhifadhi wa Urithi na Uwekezaji”.