MWENYEKITI RAJABU, TANGA NDIO CHIMBUKO LA SOKA NCHINI

Msafara wa Mapokezi ya Basi la African Sports - Tanga
English

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Rajabu Abdallah amesema mkoa huo ndio chimbuko la vilabu vya mpira nchini,hivyo wadau waunge mkono timu za eneo hilo ili kufufua ushindani uliokuwepo.

Akizungumza  wakati wa sherehe za kukabidhi basi kwaajili ya timu ya mpira wa miguu ya African Sports Club zilizofanyika makao makuu ya timu hiyo mwenyekiti Rajabu amesema timu hiyo na Coastal Union ushabiki wake ni zaidia ya Simba na Yanga.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mheshimiwa Hamis Mwinjuma amewataka mashabiki wa soka mkoani Tanga kuhakikisha wanatoa michango ya hali na mali kuweza kuweza kuziwezesha timu zao.

 

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa upande wao amezitaka timu za African Sports klabu na Coastal Union kushirikiana ili kuweza kusonga mbele.

Nae mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian amesema serikali itaendelea kutafuta maeneo kwaajili ya kujenga viwanja kwa timu hizo. Mwenyekiti Rajabu ametoa zaidi ya shilingi milioni 60 kwaajili ya kuchangia timu hizo katika shughuli mbalimbali.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.