Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Rashid Hadidi Rashid amewataka Wafanya biashara wa Eneo la Fungu refu kudumisha usafi wa mazingira ili kujikinga na Maradhi ya Mripuko.
Akizungumza katika Ziara Maalumu ya kutembelea Eneo hilo ili kuona hali ya usafi wa mazingira ya Eneo hilo, amesema ipo haja ya Wafanya biashara kudumisha usafi wa Eneo lao pamoja na Bishara zao kwani zaidi ya Wagonjwa Kumi na Tano wameripotiwa kutoka Eneo hilo
Nae Mkuu wa Wilaya Kaskazini 'A' Othman Ali Maulid amesema hali ya mazingira ya Fungu Refu hairidhishi kutokana na kuwepo kwa Viashiria mbalimbali vya Maradhi ya Mripuko na wataandaa mpango maalum wa kudumisha usafi
Meneja wa Kitengo cha Elimu ya Afya Zanzibar Bakari Hamadi Magarawa amesema kwasasa maradhi ya Mripuko wa Kipindupindu yameenea ni vyema kutumia njia za kutibu maji ikiwemo kuchemsha maji na kutia dawa
Wafanyabiashara wa Eneo hilo wamesema watahakikisha wanatumia Dawa za kutibu Maji pamoja na kusafisha Mazingira ili kujikinga na Maradhi hayo na wameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa nia ya kuwaongezea Vyoo