RC TANGA ATOA AGIZO KWA WAKUU WA WILAYA KUHUSU WAMACHINGA

Mkuu wa Mkoa Tanga
English

Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Buriani amewaagiza wakuu wa wilaya zote za eneo hilo kuwatafutia maeneo ya uhakika wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Machinga,na katafuta sehemu ambayo watakaa bila changamoto

Akizungumza wakati akifunga maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa yaliofanyika mkoani Tanga katika viwanja vya shule ya sekondari usagara kwa wiki moja Jumatatu Januari 26,2026 Balozi Batilda amesema wafanyabiashara ndogondogo wanatakiwa kuwekwa sehemu  nzuri.

Meneja wa Shirika la Bima Zanzibar Mkoa wa Tanga Hassan Abdallah  amepongeza maadhimisho hayo na kushukuru kwa shirika lao kushinda kuwa namba moja kwenye maonyesho hayo jambo ambalo limewapa faraja zaidi. Mwandikishaji wa Shiriki la Bima Zanzibar Victoria Mwafongo amesema wametembelewa na wananchi zaidi ya 800 na wamepewa elimu mbalimbali kuhusu masuala ya bima na wamenufaika nayo.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.