DC UKEREWE ATOA SIKU 14 KWA WAMILIKI WA ZANA HARAMU ZA UVUVI KUZISALIMISHA

UKEREWE

   Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Christopher Ngubiagai ametoa Siku 14 kwa Wananchi wanaomiliki zana haramu za Uvuvi zinazotumika kuvulia Samaki ndani ya Ziwa Victoria kuzisalimisha mara moja, sambamba na kuwachukulia hatua za kisheria Watumishi wa Serikali wanaoshirikiana na Wavuvi haramu kuhujumu mapato ya Halmashauri ya Wilaya hiyo.

    Agizo hilo la Serikali limetolewa katika Kikao cha Wadau wa Sekta ya Uvuvi Wilayani humo, kufuatia kushamiri wa vitendo vya Uvuvi haramu unaotishia kupungua kwa Samaki ndani ya Ziwa Victoria.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Emmanuel Shelembi amewataka Wadau wa Uvuvi Wilayani humo kushirikiana pamoja na Watendaji wa Serikali katika kukomesha Uvuvi haramu.

     Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ukerewe kimeunga mkono vita dhidi ya Uvuvi haramu iliyotangazwa na Mkuu wa Wilaya hiyo.

baadhi ya Wadau wa Sekta ya Uvuvi wameiomba Serikali kutokuwa na muhali dhidi ya vitendo vya Uvuvi haramu.

    Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mwishoni mwa Mwaka Jana ilipokea Boti Saba za Doria ili kukabiliana na Uvuvi haramu pamoja na utoroshaji wa Mazao ya Uvuvi.

    Katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha uliopita wa 2022/2023, Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe inayoundwa na Visiwa 35 katika ilikusanya zaidi ya Shilingi Bilioni Moja kama Ushuru wa Mazao ya Uvuvi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.