Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, kumchukulia hatua Mkandarasi wa mradi wa kuboresha miundombinu ya Miji Tanzania (Tactics).
Agizo hilo amelitoa kufuatia kucheleweshwa kwa mradi huo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 19.9, unaojumuisha Ujenzi wa Bararaba, Mitaro pamoja na Ujenzi wa Stendi ya Mkoa wa Manyara ambapo mpaka sasa Ujenzi wa stendi hiyo umefikia asilimia 10 tu.

Aidha Dkt. Mwigulu ameitaka Takukuru kuchunguza Ujenzi Majengo ya Hospitali ya Mji wa Babati Mrara yanayodaiwa kuweka nyufa kwa muda mfupi tu toka kukamilika kwa ujenzi huo.


Akitoa salamu za Mkoa wa Manyara Mkuu wa Mkoa Queen Sendiga amesema Mkoa wa Manyara unachangamoto ya migogoro ya ardhi hivyo kama Mkoa umeendelea kuwa na Klinik ya kutatua migogoro hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Emmanuel Khambay ameiomba Serikali ikamilishe miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo Barabara ya mrara hadi lango la kuingilia hifadhi ya Tarangire yenye urefu wa Kilomita 24.

Ziara hii ya Waziri Mkuu inamaliza LeoM koani Manyara.
