MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AKABIDHI MAGARI MAPYA NA (PA)SYSTEM KUONGEZA UFANISI KATIKA KAZI ZA HALMASHAURI
Katika juhudi za kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Ndugu John L. Kayombo, amekabidhi rasmi magari mawili mapya pamoja na mfumo wa matangazo (PA System) kwa watumishi wa Jiji la Arusha.


