WAFANYAKAZI KUMI NA TANO WA ZECO KUSIMAMISHWA KAZI KWA KUIBA UMEME.
Tabia ya Wafanyakazi wa Shirika la Umeme kujiungia Umeme bila ya kufuata utaratibu na Sheria zilizowekwa kumesababaisha baadhi ya Wafanyakazi wa shirika hilo kusimamishwa kazi kwa kupitisha uchunguzi.
Akizungumza na Wafanyakazi wa Shirika hilo Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe Shaibu Hassan Kaduara amesema kutokana na kukiuka Sheria na maadili ya kazi Shirika hilo halitomvumilia Mfanyakazi yoyote atakae bainika kuliibia Shirika ilo.