JAMII YAKUMBUSHWA KUTUNZA AFYA KWA KUFANYA MAZOEZI
Jamii imekumbushwa kuendelea kufanya Mazowezi na kutunza Mazingira ili kuimarisha afya zao.
Akizungumza mara baada ya Matembezi ya Kilomita Sita na Bonaza la Mazowezi Mlezi wa Barafu Jonging Iddi Azan amesema kufanya Mazowezi ni muhimu kwa Afya na amewataka Vijana kuacha kutumia Vileo ambavyo vinaharibu Maisha yao.
Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya Dkt. Ntuli Kapologwe amesema Wizara ya Afya inampango mkakati wa kuimarisha afya ya Jamii kwa kutumia Mabonaza ambayo yanashirikisha Jamii moja kwa moja.