WACHAMBUZI WA MICHEZO WAMZUNGUMZIA MAREHEMU MACHUPA
Mamia ya Wananchi na Wanamichezo Visiwani Zanzibar wamejitokeza kuusindikiza Mwili aliyekuwa Kocha wa makipa wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes na Taifa Stars, Marehemu Saleh Ahmed maarufu Machupa.
Marehemu Saleh Machupa, amefariki Dunia Usiku wa kuamkia Leo Juni 3, 2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.