MOROGORO KUPOTEZA ASILIMIA 10 YA MAENEO YALIYOKUWA MISITUNI
Ukataji Miti na uchomaji ovyo wa Misitu umesababisha Mkoa wa Morogoro kupoteza Asilimia 10 ya maeneo yaliyokuwa misituni huku urejeshwaji wa uoto ukiwa Asilimia 18 ya kiwango kilichofyekwa,wakati kasi ya upotevu wa Misitu ni Asilimi 81.
Maeneo ya uoto karibu Hekta 362,000 hupotea ambapo urejeshaji wake ni Hekta 66,000 hali inaonyesha ni muendelezo wa tabia ya kutumia njia za asili ambazo zinapunguza ubora na upotevu mwingi wa mazao na kuacha Ardhi wazi baada ya kukata Miti.