AKAUNTI YA NMB PESA ISIYO NA MAKATO YAZINDULIWA KANDA YA KUSINI
Benki ya NMB kanda ya kusini imezindua kampeni ya kuhamasisha na kuwawezesha watu wengi kufungua akaunti ili waweze kunufaika na faida za kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa fedha.
Kampeni hiyo inayoitwa “NMB Pesa Haachwi Mtu” kwa kanda ya kusini imezinduliwa rasmi Mkoani Lindi katika viwanja vya shule ya Msingi Mnolela halmashauri ya Mtama kwa kufanya bonanza la michezo mbalimbali.
Michezo hiyo ni pamoja na mpira wa miguu, kukimbia na magunia , kukuna nazi , kunywa soda , mpira wa pete pamoja na mazoezi ya viungo.