WAZIRI MKUU AMEOMBA USHIRIKIANO KWA WANAOKUSANYA MAONI YA DIRA MPYA YA TAIFA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, amewataka Wakuu wa Mikoa Tanzania Bara na Zanzibar kutoa ushirikiano kwa Timu za Wataalamu wanaokusanya maoni ya Dira mpya ya Taifa katika Mikoa yao ili waweze kupata maoni yenye tija kwa Taifa.
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo Jijini Dodoma wakati akifungua Semina ya Wakuu wa Mikoa wa Tanzania Bara na Zanzibara kuelekea Mchakato wa utoaji Maoni ya Dira ya Taifa ya maendeleo.=
Aidha amewataka kushirikiana na Viongozi wa Dini ili kuweza kufanikisha zoezi hilo la ukusanyaji maoni kwa Wananchi.