SUALA LA KUMKOMBOA MTOTO WA KIKE LINAHITAJI USHIRIKIANO NA JAMII.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi amesema suala la kumkomboa Mtoto wa Kike linahitaji Ushirikiano wa Taasisi zote za Umma na Binafsi na Jamii.
Akizungumza katika Viwanja vya Shamata, Wilaya ya Micheweni, kwenye hafla ya ugawaji wa Taulo za Kike kwa Wanafunzi wa Kike wa Skuli ya Sekondari ya Micheweni amesema, Mtoto wa Kike ana haki ya kupata Elimu kama Mtoto wa Kiume.