WANANCHI WA DONGE WAMETAKIWA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA MAJI
Wananchi wa Donge Meli Ishirini wametakiwa kutunza Miundombinu ya Maji safi na salama inayowekwa na Serikali pamoja na Wadhamini mbalimbali katika maeneo yao.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed ameeleza hayo wakati akizinduwa Kisima cha Maji safi na salama kilichochimbwa na wafadhili legasy aid group Foundation katika eneo la Donge Meli Ishirini.
Dk. Khalid amewanasihi Wananchi hao kuthamini juhudi hizo kwa kutunza Miundombinu hiyo ikiwemo Mfumo wa matumizi ya Nishati ya Juwa inayotumika katika uendeshaji wa Kisima hicho.