ZAIDI YA 900 MISUNGWI WAMEPATIWA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO
Zaidi ya Wakazi 900 wa Kata ya Usagara Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza wamepatiwa huduma za Matibabu ya Afya ya Kinywa na Meno zilizotolewa na wadau wa Afya katika Kituo cha Afya Usagara.
Huduma hizo zimetolewa bure kwa wakazi wa Vijiji Vitano vya Kata ya Usagara na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Tanzania Health Environment And Development Initiative Thedi na Hope Dental Centre wakati wa maadhimisho ya siku ya Afya ya Kinywa na Meno.