USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI NI KIGEZO CHA UTAWALA BORA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Mfumo wa Sema na Rais SNR ni kiungo muhimu kati ya Serikali na Wananchi na kigezo muhimu cha utawala bora unaozingatia ushirikishwaji wa Wananchi.
Dk. Mwinyi alieleza hayo katika maadhimisho ya Miaka Mitatu ya Mfumo wa Sema Na Rais Mwinyi katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.Alisema kupitia SNR, Serikali imefanikiwa kuongeza ukaribu na Wananchi kwa kuzisikiliza matatizo yanayowakabili na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.