TANZANIA KUANDIKA HISTORIA MATUMIZI YA TRENI YA UMEME
Kwa mara ya kwanza Tanzania imeandika Historia kupitia Shirika la Reli la Tanzania kwa kufanya majaribio ya kwanza ya kawaida ya Treni yake ya kisasa ya SGR inayotumia Umeme kutoka Dar Es Salaam hadi Mkoani Morogoro.
Treni hiyo ambayo ni ya kwanza kwa Afrika Mashariki inayotumia Umeme ambapo huduma Rasmi ya Safari zake zinatarajiwa kuanza Mwishoni mwa Mwezi wa Julai 2024.