SMZ KUIMARISHA HUDUMA YA MAJI KUPITIA WAHISANI

    Wizara ya Fedha na Mipango ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatarajia kupokea Euro Milioni 3 kutoka Taasisi ya Giz`3 ya Ujerumani zitakazo saidia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya Maji Visiwani Zanzibar.

   Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa (SMZ) Dkt.Juma Malik  wakati wa hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Makubaliano ya Mradi wa Maji na Taasisi ya Giz yaliyofanyika Jijini Dar-es -salaam.

KATIBU ALAANI UHARIBUFU MIUNDOMBINU YA HUDUMA ZA MAJI

     Serikali imelaani Kitendo cha hujuma za kuharibu miundombinu ya huduma za Maji safi na salama katika  Visima vya Kidutani .

     Akizungumza katika kukagua athari za kuibiwa  Waya za Umeme  katika Visima  vya Maji huko Kidutani Katibu Mkuu Wizara ya Maji Nishati na Madini Ndg.Joseph John Kilangi  amesema wizi huo unarejesha nyuma juhudi za Serikali za kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora karibu na makaazi yao . 

ZAWA YAJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO ZA UKOSEFU WA MAJI NCHINI

     Mamlaka ya Maji Zanzibar 'ZAWA' imehimizwa kuchukua hatua madhubuti  zitakayowawezesha Wananchi wa maeneo ya Mjini na Vijijini kupata huduma za Maji Safi Salama.

     Wajumbe wa Kamati ya Ardhi Mawasiliano na Nishati ya Baraza la Wawakilishi chini ya Mwenyekiti wake Mhe.Yahya Rashid Abdallah wametoa mapendekezo hayo mara baaada ya kutembelea na kupokea Taarifa ya utekekelezaji wa mradi wa kulaza mabomba Unguja na Pemba.

ZAWA YAENDELEA NA JITIHADA ZA KUREJESHA HUDUMA ZA MAJI MJINI

      Malaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) imesema inaendeelea na jitihada za kurudisha huduma ya Maji iliokosekana takriban wiki mbili ndani ya eneo la Mkoa wa Mjini.

Subscribe to #ZAWA
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.