MHE MPANGO AMESISITIZA UMUHIMU WA KUIMARISHA MIFUMO YA AFYA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema ni muhimu kuimarisha Mifumo ya Afya katika Ngazi zote hususani huduma za Afya ya Msingi ili kudhibiti hatari za Kiafya katika Jamii.
Makamu wa rais amesema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Afya Kanda ya Afrika Mashariki, kati na Kusini mwa Afrika (ECSA-HC) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini Arusha.