WAJASIRIAMALI KUREJESHA MIKOPO KWA WAKATI
Wizara ya uchumi wa Buluu na Uvuvi imehimizwa kuwasimamia Wananchi katika kurejesha Mikopo ya boti za Uvuvi inayotolewa kwa vikundi mbali mbali vya Wajasiriamali kwa lengo la kuwainua Kiuchumi ili iweze kuwanufaisha na wengine.
Wajumbe wa kamati ya Utalii Biashara na Kilimo chini ya Mwenyekiti wake Mhe Mtumwa Peya Yussuf wametoa Rai hiyo wakati wakipokea Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Wizara hiyo katika Kikao kilichowakutanisha Watendaji wa Wizara pamoja na Watendaji wa Benki ya CRDB.