WAJASIRIAMALI KUREJESHA MIKOPO KWA WAKATI

WIZARA YA UCHUMI WA BULUU NA UVUVI

Wizara ya uchumi wa Buluu na Uvuvi imehimizwa kuwasimamia Wananchi katika kurejesha Mikopo ya boti za Uvuvi inayotolewa kwa vikundi mbali mbali vya Wajasiriamali kwa lengo la kuwainua Kiuchumi ili iweze kuwanufaisha na wengine.

Wajumbe wa kamati ya Utalii Biashara na Kilimo   chini ya Mwenyekiti wake Mhe Mtumwa Peya Yussuf wametoa Rai hiyo wakati wakipokea Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Wizara hiyo katika Kikao kilichowakutanisha Watendaji wa Wizara pamoja na Watendaji wa Benki ya CRDB.

Wamesisitiza kuwepo kamati maalum itakayokuwa inashughulikia kuwahamasisha na kudai marejesho ya Mikopo hiyo katika Vikundi ambavyo vinasumbua katika kufanya marejesho ili iweze kuwapa nguvu wanaotoa Mikopo hiyo kuwasaidia na wengine.

Aidha wamewahimiza wanufaika wa Mikopo hiyo kuibua Miradi yenye Tija na inayotekelezeka ili kuweza kurejesha fedha za Mikopo pamoja na kupata faida kwa wakati.

Viongozi wa Wizara ya uchumi wa Buluu na Uvuvi wakiwasilisha Taarifa ya shughuli za Wizara hiyo wamesema Wizara imefanikiwa kuongeza uzalishaji wa Mazao ya Baharini huku wakiendelea na uhamasishaji wa Wavuvi wa Mazao hayo kurejesha Mikopo kwa wakati ili na wengine waweze kupatiwa Mikopo hiyo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.