Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewataka Wananchi kuendelea kuitunza Miundombinu inayojengwa ikiwemo ya Skuli ili kufikia malengo ya Mapinduzi ya mwaka 1964 ya kutoa elimu bure kwa Wazanzibari katika mazingira yaliyo bora zaidi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdullah ameyasema hayo alipoweka Jiwe la msingi katika ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Kiwani ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha inajenga Skuli za Ghorofa kila Wilaya na kila sehemu ambayo ina tatizo la upatikanaji wa Elimu pamoja na kuweka mazingira mazuri katika Skuli hizo ikiwemo Vifaa na rasilimali ili kuongeza ufanisi wa maendeleo ya elimu.
Aidha Mhe Hemed amesema Skuli ya Sekondari Kiwani itakapokamilika itakuwa na kiwango cha hali ya juu na Vifaa vya kisasa vya kusomea na kufundishia hivyo amewataka
Waziri wa Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Mhe Lela Mohammed Mussa amesema katika Jimbo la Kiwani kuna jumla ya Skuli nne (4) za Ghorofa za kisasa ikiwemo Skuli ya Sekondari ya Kiwani, hivyo amewataka walimu kuongeza bidii ya ufundishaji ili kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdalla amesema Ujenzi wa Mradi huo hadi kumalizika kwake itagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 6 na itatoa nafasi kwa Wanafunzi kuingia Skuli kwa Mkondo mmoja tu wa asubuhi na kupunguza msongamano wa Wanafunzi Madarasani.