RAIS SAMIA ATAKA MAMA NA BABA LISHE WAHESHIMIWE

DKT SAMIA SULUHU HASSAN
English

Rais Wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Amemtaka Waziri Wa Tamisemi Prof. Riziki Shemdoe Kutenga Na Kuyaendeleza Maeneo Yaliyo Kwisha Tengwa Kwa Ajili Ya Shughuli Za Mama Na Baba Lishe Nchini Pamoja Na Kuweka Miundombinu Bora Huku Mama Na Baba Lishe Wakitakiwa Kutumia Nishati Safi Ya Kupiki Katika Shughuli Zao.

Pia Rais Dkt Samia Ameitaka Wizara Ya Fedha Kuweka Mazingira Rafiki Ya Kisera Na Kisheria Ili Wafanyabiashara Ndogondogo Wakiwemo Mama Na Baba Lishe Nchini Waweze Kunufaika Na Mikopo Inayotolewa Na Serikali.

Rais Dkt Samia Ametoa Kauli Wakati Akifungua Kongamano La Kwanza La Kitaifa La Mama Na Baba Lishe Tanzania Lilofanyika Jijini Dar Es Salaam Na Kuwakutanisha Mama Na Baba Lishe Kutoka Tanzania Bara Na Visiwani.

Anasema Serikali Inatambua Mchango Wa Kundi Hilo Ndio Maana Wanaendelea Kuboresha Mazingira Ya Shughuli Zao Huku Akitaka Kuheshimiwa Kwa Mama Na Baba Lishe Kutokana Na Mchangano Wao Mkubwa Katika Maisha Ya Kila Siku Ya Watanzania.

Aidha Rais Dkt Samia Akatumia Fursa Hiyo Kuwataka Mama Na Baba Lishe Nchini Kuhakikisha Wanakuwa Mabalozi Wa Kulinda Amani Na Utulivu Uliopo Nchini.

Awali Waziri Wa Maendeleo Ya Jamii Jinsi Wazee Na Watoto Dkt Doroth Gwajima Anasema Lengo La Kongamano Hilo Ni Kubadilisha Uzoefu Ili Kujenga Sekta Ya Mama Na Baba Lishe Nchini.

Kwa Upande Wake Mwakilishi Wa Umoja Wa Mama Na Baba Lishe Tanzania Anasema Umoja Huo Una Wananchama Elfu Tano Kutoka Tanzania Bara Na Visiwa Lakini Wanakabiliwa Na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Ukosefu Wa Mitaji Na Mikopo Ya Masharti Nafuu Katika Kongamano Hilo Pia Rais Dkt Samia Alimkabidhi Waziri Wa Nchi, Ofisi Ya Waziri Mkuu Tawala Za Mikoa Na Serikali Za

Mitaa Tamisemi Prof Riziki Shemdoe Mfano Wa Hundi Ya Shilingi Bilioni 94 Kwa Ajili Ya Mikopo Ya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.