ONGEZEKO LA ABIRIA NA MIRUKO YA NDEGE “AAKIA” LAAKISI MAFANIKIO YA SERIKALI KATIKA KUIMARISHA USALAMA WA ANGA

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA)
English

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) kupitia Uwanja wake wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA) umeendelea kushuhudia ongezeko la idadi ya abiria pamoja na miruko ya ndege, huku hatua madhubuti za kuimarisha usalama wa anga zikiendelea kupewa kipaumbele.


 

Kwa mujibu wa takwimu za mwezi Machi 2026, jumla ya abiria 187,407 walipitia katika uwanja huo ikilinganishwa na abiria 174,654 waliorekodiwa mwezi Machi 2025. Hii ni sawa na ongezeko la abiria 12,753, jambo linaloonesha kuimarika kwa safari za anga pamoja na kuongezeka kwa mahitaji ya usafiri wa ndege kwenda na kutoka Zanzibar.


 

Katika mgawanyo wa abiria hao, abiria wa safari za ndani waliongezeka kutoka 64,887 mwezi Machi 2025 hadi kufikia 74,791 mwezi Machi 2026, wakati abiria wa safari za kimataifa waliongezeka kutoka 109,767 hadi kufikia 112,616 katika kipindi hicho. Aidha, uwanja huo umerikodi jumla ya miruko ya ndege 4,838 mwezi Machi 2026 ikilinganishwa na miruko 4,549 mwezi Machi 2025, ikiwa ni ongezeko la miruko 289.


Ongezeko hilo la shughuli za usafiri wa anga linaambatana na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha usalama wa anga unaimarishwa kwa viwango vya kimataifa, ikiwemo kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege, kuimarisha mifumo ya ukaguzi na kuongeza uwezo wa rasilimali watu wanaohusika na usalama wa anga.

Hatua hizi zinafanyika chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mh. Dr Hussein Ali Mwinyi, ambaye ameendelea kuweka mkazo katika maendeleo ya sekta ya anga kwa kuhakikisha uwekezaji unaelekezwa katika kuboresha huduma, usalama na ufanisi wa viwanja vya ndege vya Zanzibar.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.