Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dkt, Hussein Ali
Mwinyi Amewasisitiza Viongozi Wakuu Katika Taasisi Za Umma Kuzingatia Upendo,Uadilifu Na Haki Katika Kuwasimamia Wanaowaongoza Na Utekelezaji Wa Majukumu Yao.
Akizungumza Katika Kongamano La Tatu La Kiimani Kwa Viongozi Wa Serikali Lililoandaliwa Na Afisi Ya Mufti Mkuu Wa Zanzibar, Ameeleza Kuwa Kongamano Hilo Ni Msingi Wa Kukumbushana Umuhimu Wa Kuzingatia Maadili Katika Utumishi Wa Umma Na Jukwaa Muhimu La Kujifunza Uwiano Wa Kazi Kwa Misingi Ya Kiimani
Dķt, Mwinyi Ametoa Wito Kwa Viongozi Wa Umma Kutumia Kongamano Hilo Kama Dira Ya Kusimamia Majukumu Yao Kwa Wema ,Uadilifu ,Haki Na Busara Na Kuzingatia Kuwa Uongozi Ni Dhamana.
Amebainisha Kuwa Maeneo Yanayofanya Vizuri Katika Utumishi Wa Umma Ni Yale Yenye Upendo Na Utekelezaji Wa Haki ,Uadilifu Na Uwajibikaji Na Kwahimiza Viongozi Kuwa Waadilifu Na Amewataka Viongozi Kuyapokea Maelekezo Ya Mashehe Kama Nyenzo Ya Kubadilika Katika Utekelezaji Wa Majukumu
