Wafanyabiashara wa Soko la Kinyasini Wilaya ya Kaskazini 'a' Unguja wamesema kuwa Eneo la Soko ni dogo kwa kufanyia biashara zao na linasababisha msongamano baina ya Wafanyabiashra na Wateja.
Wakizungumza na Kamera ya Biashara na Uchumi ZBC Wafanyabiashara hao wamesema Soko hilo halikidhi kuchukua Watu wengi hali inayopelekea baadhi ya Wafanyabiashara kupanga bidhaa chini na pembezoni mwa barabara.



Kutokana na hali halisi ya Sokoni hapo Wafanyabiashara wametumia kipaza sauti cha ZBC kuiomba Serikali kulitazama hilo na kuchukua hatua ambazo zitawafanya wao kupata Eneo kubwa katika mazingira rafiki na salama ya kuuza bidhaa zao.
Kwa upande wake Mkuu wa Soko la Kinyasini Ndg.Arafa Mohamed ametoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya Wafanyabiashara kukosa Eneo la kutosha kufanyia biashara zao na kusema Serikali inatambua hilo na tayari hatua stahiki zimechukuliwa za Ujenzi wa Soko jingine ambalo litakuwa lina hadhi ya kisasa na kuwanufaisha Wananchi wote wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
