HUDUMA ZA KIBINGWA 20 ZATOLEWA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA

RAIS DKT.MWINYI
English

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa mageuzi namafanikio makubwa ya utoaji wa huduma za matibabu ya kibingwa kwa Wananchi. 

Akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Prof. Abel Makubi akiambatana na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar Dķt.Mwinyi amesifia huduma hizo ikiwemo matibabu ya Figo ,Moyo na Ubongo kufanyika hapa Nchini ,hatua aliyopunguzia Serikali na Wananchi gharama za kuwapeleka Wagonjwa Nje ya Nchi.

Aidha Rais Dķt.Mwinyi ameushauri Uongozi wa Hosptali ya Benjamin Mkapa kuendeleza utaratibu wa Matibabu nje kwa kuwafikia Wananchi katika maeneo yao kwani unasaidia kuwatibu Watu wengi zaidi kwa wakati mmoja.

 

Aidha Dķt.Mwinyi ameahidi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya Zanzibar itaendeleza ushirikiano na Hosptali ya Benjamin Mkapa na kutafuta njia bora za kufanya kazi kwa pamoja na kuipongeza kwa kuendeleza mafunzo ya kuwajengea uwezo Watendaji kupitia Taasisi za ndani na Wadau kutoka Nje ya Nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Prof, Abel Makubi ameeleza kuwa Hospitali imepata mafanikio makubwa katika Miaka Kumi tangu kuanzishwa kwake kwa kutoa matibabu ya huduma za kibingwa 20 ikiwemo matibabu ya upandikizaji wa Figo ,Upasuaji wa Ubongo na Matibabu ya Moyo kulikochangiwa na Serikali kufanya Mageuzi makubwa katika Sekta ya Afya .

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.