Akitangaza Wadhamini wa Tamasha hilo Mwenyekiti wa Tamasha Mahfoudh Said Omar, huko Hoteli ya Kwaza Kizimkazi amesema Maandalizi ya Tamasha hilo yanaendelea vizuri ambapo Mwaka huu litakuwa bora zaidi kuliko Matamasha yote yaliopita.
Amesema Tamasha hilo litahusisha Shughuli mbalimbali za Kimaendeleo, Kiuchumi na Kiutamaduni ambapo pia litahusisha Uzinduzi wa Miradi ya Maendeleo ikiwemo Ufunguzi wa Skuli ya Tasani Makunduchi na Jengo la Afya la Huduma ya Mama na Mtoto huko Kizimkazi.
Balozi wa Tamasha la Kizimkazi Day Doto Abdalla amewaomba Wageni na Wenyeji kushiriki katika Tamasha hilo kwa ajili ya kujionea na kujifunza mambo mbali mbali ya yakiwemo Mila Silka na Utamaduni.
Tamasha hilo ambalo linatarajiwa Kufungwa Agosti 25 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan limedhaminiwa na Taasisi mbali mbali zikiwemo Benki, Kampuni ya Simu ya TTCL, Tigo-Zantel na Mwanawake Invitative