ZBC imezungumza na Mussa Juma Issa ambae ni Mtoto kati ya Watoto Watano wa Marehemu Juma Issa Noura ambae ni msimamizi wa Mirathi hiyo yenye Jarada Namba Nne Mwaka 2009
Amesema kwa Muda Mrefu kumekuwa na sintofahamu ya kupata Mirathi yao ikiwemo Maeneo ya Ardhi yaliyopo Jambiani na Makunduchi licha ya kufungua Madai ya Mirathi katika Ofisi ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana
Kufuatia Malalamiko hayo ZBC imemtafuta Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Ndg.Abdallah Twalib Abdallah ili kupata ufafanuzi wa jambo hilo ambapo ameeleza kuwa kukwama kwa Mchakato wa Mirathi unatokana na Warithi kushindwa kuthibitisha uhalali wa Mali wanazodai kuachwa na Baba yao
Hadi ZBC inaripoti Taarifa hii tayari Baadhi ya Maeneo yanayodaiwa kumilikiwa na Marehemu Juma Issa Noura yameanza Ujenzi hali inayoleta ukakasi kwa Warithi