Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria utumishi na Utawala bora Mh Haroun Ali Suleiman ameitaka Tume ya haki za Binaadamu na utawala bora Tanzania kuwa makini katika kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu utekelezaji wa mpango kazi wa haki za Binaadamu na Biashara Zanzibar.
Akizungumza na Watendaji wa Tume hiyo huko Ofisini kwake Mazizini amesema kufikia malengo la Ziara hiyo ni kutafuta maoni ya Wananchi wenyewe badala ya Viongozi ili kufanikisha vyema mpango huo
Mohd Khamiss Hamad ambae ni Makamo Mwenyekiti wa Tume ya haki za Binaadamu na Utawala bora amesema kuwa lengo kuu la Mpango kazi huo ni kuweza kutatua matatizo ya Kiuchumi na Biashara yanayowakabili Wananchi katika Jamii.
Katibu Mtendaji Tume hiyo Patience Ntwina amesema wanakusudia kuwafikia Wadau wa Uchumi wa Buluu, Utali na Nishati ili kuweza kuimarisha utekelezaji na utendaji wa haki za Binaadamu