Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab amesema ameridhishwa na Matenegenezo ya jengo la Raha leo ambalo linatarajiwa kuwa Makao Makuu ya Shirika la Utangazaji Zanzibar.
Ameyasema hayo wakati akifanya Ukagua katika Jengo la Raha Leo lililotenegenzwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ambapo amesema hatua hiyo itasaidia kuimarisha utendaji kazi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar pamoja na kulitaka Shirika hilo kutunza mazingira na Miundombinu ya Jengo hili.
Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Ramadhan Athuman Bukini amesema Jengo la Raha Leo litasaidia kutimiza malengo ya Shirika kwa kuwa na Makao Makuu yatakayojumuisha Idara zote zilizokuwa katika Shirika hilo
stories
standard