Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Shaibu Hassan Kaduara amesema Wizara yake itahakikisha inamaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji Zanzibar.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Mifumo wa usimamizi wa Maji Tazama Maji katika Ukumbi wa Zawa Madema amesema hatua hiyo itaweza kuijulisha Mamlaka sehemu yenye kima kidogo ama kikubwa cha Maji na kutafutiwa ufumbuzi wake.
Waziri Kaduara amesema hatua hiyo itaiwezesha Zawa kuunganisha Mifumo yake ya Taarifa katika Maeneo tofauti ya Maji na kutuoa huduma bora kwao .
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Zawa Dkt .Salha Muhammed Kassim amesema Mifumo huo wa Kisasa utasaidia kuzijua sehemu mahsusi zilizo na Maji katika Maeneo ya vianzio vya upatikanaji wa Visima vya Maji viwe vya Mamlaka au vya Mtu Binafsi
Mfumo huo uliofanywa ni kwa mashirikiano ya Mamlaka ya Maji Jeica , kutoka Japan , na Watalamu kutoka Nchini Kenya.