Mhadhiri wa Kimataifa wa dini ya Kiislamu Dk. Sheikh Seif Hassan Sulleiman amemtaja Rais Samia Suluhu Hassan kama mmoja wa viongozi wa mfano na kuigwa Duniani katika Diplomasia ya kisiasa.
Ni katika Viwanja vya furahisha Jijini Mwanza, ambako Waumini wa Dini ya Kiislamu Wanashiriki kongamano la Siku Kumi la Maadili na unasihi lililoandaliwa na Baraza kuu la Waislamu Tanzania Bakwata Mkoani hapa.
Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo ni Mhadhiri wa kimataifa wa Dini ya kiislamu Sheikh Dkt. Seif Hassan Sulle kutoka Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa mwanza, said mohammed mtanda anasema Viongozi wa Dini wanayo haki na wajibu wa kuiombea Tanzania na Viongozi wake ili wasiyumbe, huku akieleza namna Serikali iliyotekeleza Miradi ya kimkakati katika Mkoa wa Mwanza.
Kongamano hilo limetanguliwa na Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu 1446 Hijilia, ambapo Waumini wamepata Elimu ya magonjwa mbalimbali ikiwemo Saratani ya Saratani ya Matiti na Fistula kwa akinamama pamoja na Bakwata kuzindua Kampeni ya upandaji Miti 175,000.