SMZ HAIJARIDHISHWA NA UJENZI WA SKULI YA SEKONDARI YA MAKUNDUCHI

MAKAMO WA PILI

    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali haijaridhishwa na kasi ya Ujenzi unaoendelea wa Skuli ya Sekondari ya Makunduchi jambo linalorejesha nyuma dhamira ya Dkt. Mwinyi ya kuhakikisha anaondoa matatizo zote kwa Wananchi ikiwemo Elimu kwa Wanafuzi wa Mikoa yote ya Zanzibar.

   Ameyasema hayo alipokagua Ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake ya kuitembelea Skuli hiyo kila Mwezi.

    Amesema Serikali imeshailipa Kampuni ya Fuchs Contraction Limited zaidi ya Shiling Bilioni 4 ili kuharakisha kumalizika kwa Ujenzi huo lakini endapo Kampuni hiyo atashindwa kumaliza kwa wakati waliokubaliana itakuwa wamejinyima fursa ya kufanya kazi  Zanzibar hasa katika Kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nane.

    Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Ali Abdulghulam Hussein amesema Wizara imejipanga kuhakikisha inaipatia kila Skuli  Vifaa vya kusomea vya kisasa ili kuimarisha Mfumo wa Elimu Zanzibar ambapo kwa sasa Wizara imefanya ununuzi wa Vifaa mbali mbali ikiwemo Vitanda, Kompyuta, Projecta, Viti na Meza.

   Nae Mkandarasi kutoka Kampuni ya Fuchs Contraction Ltd Devid Mwasomola ametaja sababu ya kushindwa kuendelea na Ujenzi wa Skuli hiyo ni kukosekana kwa nondo na malipo kwa Wafanyakazi hivyo ameahidi kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa.

   Katika Ziara hiyo pia Mhe.Hemed amefika katika Skuli ya Sekondari ya Hasnuu Makame na kukagua matengenezo ya Jengo la Dahalia ya Wanawake liloungua moto na kuuagiza Uongozi wa Wizara ya Elimu kuhakikisha wanaijengea Uzio Skuli hio ili kuimarisha ulinzi na usalama kwa Wanafunzi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.