TEHAMA KUTUMIKA KATIKA UTUNZAJI NA USIMAMIZI WA KUMBUKUMBU AFRIKA

KUMBUKUMBU TEHEMA

    Mfumo wa Utunzaji Kumbukumbu kwa kieletroniki utazisaidia Taasisi za Umma na Binafsi kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia katika kukuza uchumi wa Afrika Kidigitali.

    Akifunga Mafunzo ya Kurikodi Kumbukumbu na Nyaraka Kidigitali kwa Washiriki wa Mkutano wa RMFA Makamu Mkuu wa Chuo cha Taifa Zanzibar (SUZA) Prof. Makame Mohamed Haji amesema kulingana na Wakati uliopo ni muhimu kwa Sekta mbali mbali kutumia Tehama ili kusaidia kukuza Uchumi wa Nchi na Afrika kwa ujumla.

    Washiriki wa Mkutano huo wamesema Mafunzo waliyoyapata yamewajengea uwezo wa kutambua na kuhifadhi kumbukumbu kidigitali na mbinu za kutatua matatizo wanayokutana nayo katika kutumia mfumo mpya wa uhifadhi wa kumbukumbu. 

   Mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya usimamizi wa Kumbukumbu Afrika (RMFA) yenye Makao Makuu yake Nchini Uganda na umewakutanisha Washiriki kutoka Afrika Kusini, Mashariki na Magharibi. 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.