Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani ipu Dkt Tulia Akson ameongoza Kikao cha Kamati ya Uongozi wa Umoja huo unaofanyika Zanzibar ambacho kitajadili Maandalizi ya Mkutano wa IPU unaotarajiwa kufanyika Mwezi wa Kumi Mwaka huu.
Dkt Tulia Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuaanza Kikao hicho huko Kizimkazi amesema Kikao hicho pia kitajadili taratibu mbalimbali ambazo zinahitaji kubadilishwa ndani ya ipu pamoana na changamoto za baadhi ya Nchi za Afrika ambazo hazinufaiki na umoja huo.
Dkt Tulia amesema Kikao hicho kinakutana kuratibu Mkutano wa Mwaka ambao utahusisha zaidi ya Wabunge Elfu Mbili kutoka Mabunge 180 Duniani ambao utafanyika Nchini Uswizi.
Aidha amesema Mkutano huo pia utajadili mambo mbalimbali ikiwemo Sera zinazohusu usumbufu wa Kijinsia na Madhara yake pamoja na kujadili fursa za msingi hasa kwa Mabunge ya Afrika.