Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kujiepusha na Vitendo vinavyoenda tofauti na Mila na Desturi za Tanzania na kuendelea kulinda Amani na utulivu uliopo Nchini.
Waziri mkuu Majaliwa maetoa Kauli hiyo kwenye Baraza la Eid El Adh’haa Kitaifa lililofanyika katika Msikiti wa Mfalme Mohammed Vi Makamo Makuu ya Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA) Kinondoni Jijini Dar es salaam mara baada ya kukamilika kwa swala Sikukuu ya Eid El Adh’haa.
Amesema mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanaondoa misingi ya Malezi hivyo kama nchi hatuna budi ya kuimarisha taasisi za malezi ili kuwa na taifa lenye Maadili bora
Pia Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa akatumia fursa hiyo kuwataka Watanzania kujitokeza kushiriki katika Uchaguzi wa serikali za Mitaa mwishoni mwa Mwaka.
Nae kaimu mufti wa tanzania sheikh ali khamis ngeruko amesema changamoto nyingi katika jamii hasa katika ndoa na watu kuuana ni matokeo ya kukosekana kwa afya ya akili ndani ya jamii.
Awali akituoa Khuba sikuu hiyo Sheikh Ally Mubarak amewataka waumini wa Dini ya Kiislamu kuitumia Siku hiyo kwa ajili ya kuwakumbuka Watu wenye mahitaji katika Jamii.